WENGI WANAISHI KWA KUSADIKIKA SABABU YA KUFANYIWA MAAMUZI
Hali ya umasikini wa kipato miongoni mwa wananchi katika nchi za ulimwengu wa tatu inachangia upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii kuwa ngumu na kuwa kikwazo kikubwa cha kujiamulia mambo yanayowahusu.
Hayo yamebainika wazi wakati wa wiki ya kampeni ya kupiga vita umasikini na kudai nafasi zaidi ya kujiamulia mambo ya maendeleo kuanzia ngazi za chini, maarufu kwa jina la GCAP, hususan katika nchi changa.
Ni wazi kuwa vyombo vikubwa vya kibepari, haswa taasisi za kifedha washirika wa Bretton Woods iliyoanzia nchini Marekani zimekua na tabia ya kuweka masharti kadha wa kadha yanayolenga kuzibeba nchi tajiri na kuzikandamiza zile masikini, (developing countries) pale zinapoamua kuomba misaada mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi.
Moja ya masharti ambayo yamewagusa wananchi wengi ni fagio la kupunguzwa kazi, hii imetokana na mambo mbalimbali, serikali za nchi changa kushurutishwa kuwa na idadi ndogo ya wafanyakazi na kujitoa katika majukumu mbalimbali ya kiuchumi, ubinafsishaji, serikali kutojihusisha na biashara mojamoja na kufuata taratibu za soko huria (market economy).
Bw. Audax Rukonge mkazi wa jijini Dar es salaam anasema kuwa mizizi ya umasikini inaletwa na mifumo ambayo siyo shirikishi, yaani wananchi kutojulishwa chochote au kutoshiriki katika maamuzi ambayo yanawagusa kwa namna moja au nyingine kimaisha.
“hii ni moja ya sababu inayochangia kwa kiasi kikubwa umasikini katika nchi zetu” anasema Bw. Rukonge ambaye ni mtaalam wa masuala ya kilimo akitoa mfano kuwa katika zoezi la kupunguza wafanyakazi sekta nyingi zimeadhirika ikiwamo ile ya kilimo ambapo kwa kukosa wataalam wa kuwasaidia wakulima katika kilimo cha kisasa tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 18 ya watu hawana uhakika wa chakula, kilimo wanachoshiriki ni kile cha bora liende.
Rukonge ambaye pia ni mtafiti katika asasi ya kimataifa isiyokuwa ya kiserikali iitwayo Action Aid anaongeza kuwa ili kushughulikia tabia hii ya mifumo ya ushauri kutoka nje anasema ipo haja ya viongozi kutoka katika nchi changa za ulimwengu wa tatu kupigania haki ya nchi zao kupata nafasi zaidi ya kupiga kura katika maamuzi na kuchangia kubadili sera za mashirika makubwa ya misaada.
“ asasi zisizo za kiserikali zinasaidia kuwafumbua wananchi macho na kuweka shinikizo zaidi ili milango ya kafanya maamuzi wao wenyewe iwepo” anasema Rukonge na kuongeza kuwa katika mkutano uliofanyika nchini Singapore mwezi uliopita mchango wa asasi hizo umeonekana.
Rukonge anatolea mfano wa mafanikio hayo ni upatikanaji bure wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa usio na tiba wa UKIMWI ambao umesababisha upotevu wa nguvu kazi kubwa katika nchi zinazoendelea, mfano katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Sub Saharan Africa, umesababisha yatima zaidi ya milioni mbili.
Hata hivyo, anaonya kuwa haina maana hata kidogo kwa taasisi kubwa za kifedha zinazotoa misaada katika nchi mbalimbali zinazoendelea kudai uchumi wa nchi fulani umekua kwa kiwango cha kuridhisha wakati mwananchi wa kawaida hata hajapata mabadiliko yoyote katika mfumo wake wa maisha ya kila siku, zaidi ya kuongezeka kwa gharama za maisha kila kukicha ambazo ni mzigo.
Pamoja na hayo, Lawrent Wambura, mtafiti na mshauri wa masuala ya UKIMWI anasema nchi nyingi changa ikiwemo Tanzania zimekuwa zikipata fedha kupitia masharti ya Shirika la Fedha la Dunia (IMF) na Benki ya Dunia (WB) ili kupambana na umasikini.
Hata hivyo, anaongeza kwa kusema kuwa tafiti zinaonyesha kuwa huduma mbalimbali na mategemeo ya kuishi miongoni mwa wananchi wengi wa nchi za ulimwengu wa tatu yamepungua. Takwimu zinaonyesha kuwa katika miaka ya tisini kati ya watoto 1000 waliozaliwa, 100 kati yao walipoteza maisha katika hatua za awali kabisa za maisha yao duniani, lakini kuna dalili za wazi kuwa hali hiyo inaendelea kukua kutokana na ukosefu wa huduma madhubuti.
Bw. Wambura anasema kuwa sio jambo la kushangaza kumkuta mgonjwa katika maeneo ya vijijini akitembea umbali mrefu ili kufuata huduma ya afya, tena huduma yenyewe inayofungiwa safari ni ya kusuasua kwa kuwa hakuna vifaa vinavyohitajika.
Mtaalam huyo anasema kuwa kutokana na hali hiyo baadhi ya wagonjwa hushauriwa kurudi nyumbani na kufuata matokeo na majibu ya maabara kuhusu magonjwa yanayowasumbua kesho yake, hali ambayo huwazidishia zaidi maumivu na kuhatarisha maisha yao, pengine kifo.
Pamoja na hayo anasema kuwa suala la uchangiaji wa gharama mbalimbali za afya umekuwa kikwazo kikubwa katika upatikanaji wa huduma ya afya kwa wananchi wengi wasio na uwezo kwa kuwa hali yao kimapato sio nzuri ili kujigharamia.
Naye Albert Memba ambaye ni mwandishi, pia mhamasishaji wa masuala mbalimbali ya kijamii anasema kuwa ingawa huduma nyingi zimekuwa zikifanyiwa marekebisho ipo haja ya kuhakikisha kuwa wataalam wanapatikana kwa idadi ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya jamii.
Anasema kuwa tafiti iliyofanyika hivi karibuni inaonyesha kuwa takriban asilimia 70 ya misaada ya kifedha kwa nchi changa imekuwa ikirudi huko ilikotoka kwa njia mbalimbali kutokana na udhaifu uliopo katika nchi changa, au kusababishwa na umakini dhaifu katika kuingia mikataba mbalimbali na nchi tajiri.
Anasema asilimia hiyo 70 imekuwa ikirudi ilikotoka kupitia mfumo wa kuwalipa wataalamu na washauri kutoka nchi zilizoendela, ununuaji wa mashine za kisasa na vipuri vyake, au kuhamisha teknolojia (Horizontal Technology Transfer) pamoja na mafundi wa mashine hizo ambao inadaiwa utaalamu wao haupatikani katika nchi za ulimwengu wa tatu.
“ni wazi kuwa misaada ya namna hii hailengi katika kuboresha hali ya maisha ya watu kwa kuwa hata hao wanaotoa misaada huwa hawawi wazi na kusema asilimia fulani tutaichukua” anasema Memba na kuongeza kuwa ni vema wananchi ambao ndio waathirika wakubwa hasa pale mambo yanapoenda vibaya wawekwe wazi ili waamue wenyewe na sio mtu mwingine awaamulie.
Anasisitiza kuwa lazima nchi changa ziwe ‘masikini jeuri’ pia ipo haja ya kuhakikisha kuwa wataalamu wanapatika kwa nguvu zote, husasan walimu ambao bado hawatoshelezi mahitaji ya wanafunzi hapa nchini kwa kuwa idadi ya wanafunzi inaongezeka kila kukicha.
Memba anasema bila kuwa na msingi madhubuti wa elimu maamuzi mengi yatafanywa na nguvu za nje kwa kuwa uwezo wa kung’amua ubaya au uzuri wa kuingia katika mikataba mbalimbali miongoni mwa wananchi wa nchi changa au viongozi wao utazidi kuwa mdogo na wenye shaka kubwa.
Ni wazi kuwa baadhi ya bidhaa zisizo na viwango zimekuwa zikitupwa katika soko la nchi changa kwa kisingizio cha soko huria, bidhaa hizo ‘junk products’, zimekuwa chanzo cha matatizo mengi kijamii. Mfano magonjwa mbalimbali, mapema mwaka huu mtafiti mmoja alianishisha kuwa mipira ya kike ya kujikinga kwa UKIMWI haina viwango vya kimataifa vivyotambulika, ISO, hivyo kuweka katika mashaka maisha ya watumiaji wake, ni hatari zaidi kwa kuwa bidhaa za sampuli hii nyingine hutolewa bure kwa kisingizio cha kuokoa maisha.
Ni jambo lililo wazi kuwa bila kuwa na mshikamo madhubiti miongoni mwa wananchi na viongozi mageuzi ya kiuchumi hayawezi kutimia na kumkomboa mtu wa kawaida. Ni vigumu kuwaamulia wananchi jambo fulani ili wao walitekeleze bila kuwashirikisha. Ushirikishwaji wa wananchi katika mambo yanayowagusa ni muhimu ili kupata maendeleo endelevu.
MWISHO.